Kikosi cha Clube Deportivo 1° de Agosto kimeanza safari ya kuelekea Dar es salaam, Tanzania tayari kwa michezo miwili ya hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC.

Shirikisho la soka barani Afrika ‘CAF’ limeamuru michezo yote miwili kwa timu hizo ichezwe jijini Dar es salaam, kufuatia kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mchezo wa kwanza uliokuwa uchezwe Februari 14 nchini Angola.

Michezo yote miwili imetakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na iwe imechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, CD 1 Agosto watakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mchezo huo.

May be an image of one or more people and people standing
May be an image of one or more people and people standing
May be an image of one or more people, people standing and outdoors
May be an image of 1 person
Rais Magufuli amlilia Balozi Kijazi, asisitiza maombi
‘TOTAL WAR, POINT OF NO RETURN’ kuimaliza Al Ahly Dar