Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, amezuru Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli, wakati aliposimama kwa muda wilayani Chato alipokuwa njiani kuelekea wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Mpango ameenda Kigoma kwa ajili ya kufunga Kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM), za Jimbo la Muhambwe kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Kiti cha Ubunge unaotarajiwa kufanyika Jumapili Mei 16, 2021 kufuatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hayati Nditye.

Dk. Mpango, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Mei 14, 2021.
Mahakama ya Juu yazuia pendekezo la kubadilisha katiba
Exclusive: Gharama kubwa za matibabu zachangia matumizi holela ya dawa, "inaua kwa haraka sana"