Ujio wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis nchini Kenya uliacha historia kubwa nchini humo huku rais wa nchi hiyo pia akitaka kumuachia kumbukumbu nzuri kiongozi huyo.

Papa Francis aliingia nchini humo na kupokelewa na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta aliyeambatana mkewe Magreth pamoja na viongozi wengine wa dini, vyama na serikali katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Baba Mtakatifu alifika katika ikulu ya Kenya ambapo alikabidhiwa zawadi ya kipekee inayoendana na sifa yake ya kutopenda makuu.

Uhuru akiwa na mkewe walimkabidhi mchoro wenye picha ya vivutio vya utalii ambavyo Mungu ameijalia Kenya kama inavyoonekana hapo chini.

ZAWADI YA Kenyatta

 

Lowassa Awatahadharisha Polisi Kifo Cha Mawazo, Mbowe Kufungua Kesi Nyingine
Jenerali Ulimwengu Amshauri Rais Magufuli ili Afanikiwe Kipindi Chote