Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amewashangaza mashabiki wa soka nchini humo na kwingineko duniani, kufuatia kuonekana akijivinjari katika mitaa ya katikati ya jiji la London, usiku wa kuamkia jana.

Wilshere, amewaacha mashabiki wa soka katika mshangao huo, kutokana na hali yake kimwili, kuhitaji kupumzika, kufuatia jeraha la mguu ambalo lilimuweka nje ya uwanja tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Hata hivyo mwishoni mwa juma lililopita alianza mazoei na wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Arsenal, lakini jambo hilo halimpi nafasi ya kuanza kutoka na kwenda katika kumbi za starehe.

Mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Daily Mail amemnasa kiungo huyo akiwa katika moja ya mitaa ya jiji la London mishale ya usiku wa saa nane na robo na mbaya zaidi alikua akihojiwa na askari polisi.

Polisi wamethibitisha kumfanya mahojiano na Wilshere, katika maeneo ya London West End nightspot Cafe de Paris, baada ya kwenda kinyume na taratibu.

Mpiga picha wa gazeti la Daily Mail, alijitahidi kumpiga picha mchezaji huyo kwa kificho na kufanikiwa kupata uthibitisho kuwa ni Wilshere, ambaye alistahili kuwa nyumbani kwa mapumziko.

Wilshere covers his face with his jacket as he speaks to a police officer in central London 

Mwanzo Wilshere alionekana kama kushtuka na kufikia hatua ya kujifunika la koti alilokua amevaa, kitendo mbacho kiliendelea kumpa ujasiri mpiga picha kwa kupiga picha nyingine kadhaa.

Wilshere, anapewa nafasi kubwa ya kuwa katika kikosi cha Arsenal mbacho kitamalizia sehemu ya msimu huu na kisha kujumuishwa katika kundi la wachezaji wa timu ya taifa ya England ambao watakwenda kushiriki fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2016 (Euro 2016), zitakazofanyika nchini Ufaransa kuanzia mwezi Juni.

Wilshere, amekua na matukio tofauti na utovu wa nidhamu anapokua nje ya uwanja, na tayari meneja wa klabu ya Arsenal wameshaonyesha kuchukizwa na moja ya mambo anayoyafanya hadi ikapelekea mchezaji huyo kuomba radhi hadharani.

Baadhi Ya Matukio Ya Utovu Wa Nidhamu Aliyowahi Kuyafanya Jack Wilshere Tangu Mwaka 2010.

Wilshere was arrested for assault after a brawl outside a nightclub and eventually cautioned in 20102010: Alikamatwa na polisi baada ya kuonekana akipigana nje ya ukumbi wa starehe jijini London.

2011: Alikubalia kosa na kupewa onyo kali na jeshi la polisi, baada ya kumtemea mate dereva wa teksi aliyekua amevaa kofia yenye nembo ya klabu ya Tottenham Hotspur.

2012: Alionywa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), baada ya kuandika utabiri wa moja ya michezo ya klabu ya Arsenal katika mtandao wa kijamii wa tweeter.

2013: Alifungiwa kucheza michezo miwili baada ya kuwaonyesha ishara ya kidole cha kati mashabiki wa klabu ya Man City.

2013: Alionekana akivuta sigara hadharani nje ya ukumbi wa starehe huko jijini London.

2014: Kituo cha televisheni cha Sky, kilimlazimisha kuomba radhi baada ya kuikebehi klabu ya Tottenham, wakati wa sherehe za kutembeza kombe la FA katika baadhi ya barabara za jijini London.

Wilshere was spotted smoking in a Las Vegas swimming pool in 2014 after England’s World Cup exit2014: Alionekana akivuta siraga akiwa katika bwawa la kuogelea huko Las Vegas nchini Marekani, siku chache baada ya timu ya taifa ya England kutolewa kwenye fainali za kombe la dunia.

Wilshere was caught on camera holding a shisha pipe at a London nightclub in 20152015: Alionekana akiwa ameshika mrija wa kuvutia shisha akiwa kwenye ukumbi wa starehe jijini London.

Wilshere apologised after leading a foul-mouthed anti-Tottenham chant during an FA Cup victory parade2015: Aliomba radhi baada ya kuikebehi hadharani klabu ya Tottenham, wakati wa sherehe za kutembeza kombe la FA katika baadhi ya barabara za jijini London.

Darasa la Saba waiponza TTCL, ATCL yaligharimu Taifa
Chelsea Kukutana Na Antonio Conte Magharibi Mwa London