Kocha Mkuu Mpya wa Klabu ya Simba SC Franco Pablo Martin amekutana na Wasaidizi wake Hitimana Thiery na Selemen Matola kwa mara ya kwanza kambini.

Kocha Martin Alifika Kambini leo Alhamis (Novemba 10) jioni, kabla ya kikosi cha Simba SC hakijaelekea mazoezini kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19, Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha Franco aliwasili jijini Dar es salaam asubuhi na kupokewa na Mratibu wa Simba SC Abbas Haji.

Kocha Franko akisalimiana na Kocha Msaidizi Hitimana Thiery
Kocha Franco akisalimiana na Kocha Msaidizi Seleman Matola
Kocha Franco alipowasili kambini leo jioni
Kocha Franco akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara gonzalez na meneja wa timu Patrick Rweyemamu
Kocha Franco akiwasili Kambini leo jioni

Bilioni 688 zimetumika kuboresha huduma za maji vijijini
Serikali yazindua mkakati wa kutokomeza ukeketaji