Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa jana aliteka jiji la Tanga ambalo linaaminika kuwa kitovu cha CCM na moja kati ya ngome kubwa za chama hicho ambayo haijawahi kuongozwa na upinzani katika majimbo yake yote.

Katika hali ambayo wengi hawakutarajia, maelfu ya watu walifurika jana katika uwanja wa Tangamano kwa lengo la kumsikiliza  ambapo inadaiwa kuwa mafuriko hayo yalimshinda na kuamua kukatisha mkutano baada ya mamia ya watu kuanza kupoteza fahamu kutokana na msongamano huo.

Duru kutoka jijini humo zinaeleza kuwa watu walianza kufurika kuanzia asubuhi na kufikia mchana, helkopta ya mgombea huyo ilishindwa kutua katika eneo hilo kutokana na msongamano wa watu na kulazimika kushuka eneo lingine na kuchukua gari hadi katika eneo hilo.

Inaelezwa kuwa barabara zote kubwa za jiji hilo zilifurika, paa za majengo na miti iliyokuwa katika eneo hilo pia viligueka kuwa msaada wa eneo la mafuriko hayo hali iliyopelekea barabara ya Tiafa inayounganisha jiji hilo na vitongoji vyake kufungwa ili kuepusha ajali.

Tanga 2

Baada ya jitihada za viongozi wa Chadema na Ukawa kujaribu kuwatuliza watu hao kushindikana, Lowassa alichukua dakika chache kuwaomba kura wananchi hao na kuwaomba kurudi majumbani kutokana na hali iliyojitokeza ili kuepusha maafa.

Wakati wananchi hao wanarudi majumbani kwao, polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya maelfu ya watu waliojaa kwenye barabara baadhi ya jiji hilo.

Tanga 3

Magufuli Awanyooshea Kidole Wawekezaji Iringa
Anna Mghwira Awataka Wananchi Kuzikataa Sinema Za CCM