Edward Lowassa anazidi kuzihesabu kilometa akipita katika maeneo mbalimbali nchini kuwashawishi wananchi kumchagua kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano ambapo leo ametikisa jimbo la Mtama, ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Nape Nnauye anagombea ubunge.
Mgombea huyo wa Chadema ambaye aliingia katika jimbo hilo kwa chopa akiwa na meneja kampeni wa Ukawa, Frederick Sumaye pamoja na viongozi wengine, alilakiwa na maelfu ya wakazi wa eneo hilo.

Wakazi wa Mtama wakiwa juu ya paa la nyumba wakiishangilia Chopa iliyombeba Lowassa
Lowassa na timu yake ya Ukawa wamefanya mkutano mkubwa katika eneo hilo na kupokea maelfu ya kadi za wananchama wa CCM walioamua kujiunga na vuguvugu la mabadiliko kupitia Chadema.