Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, anaeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameendelea kutikisa eneo la Kanda ya Ziwa ambapo jana alipata mapokezi ya kihistoria jijini Mwanza.

Wafuasi wa Ukawa walianza kumiminika katika viwanja vya Furahisha kuanzia majira ya asubuhi kumsubiri Lowassa aliyeambatana na wafuasi wengine wa Ukawa huku mafuriko ya watu yakianza kuoenekana kwenye barabara zote zinazoelekea katika eneo la tukio.

Kama ilivyokuwa kwa Musoma, vijana wa jiji hilo walionekana wakifanya usafi kwenye barabara za jiji hilo wakideki sehemu ambazo Lowassa alipangiwa kupita. Vijana hao walimpokea kwa wingi katika uwanja wa ndege na kufunga barabara za Ilemela na Kitangili. Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Ukawa katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo, wingi wa watu hao uliwazidia polisi ambao waliamua kuwaacha waendelee na zoezi lao kwa amani.

Hatimaye, Lowassa na viongozi wa ngome ya Ukawa waliingia katika viwanja vya Furahisha na kulakiwa na ‘mafuriko’ ya watu ambayo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyaita ‘Bahari’.

Viongozi wa Ukawa, pamoja na wazungumzaji wengine wakuu wa ngome hiyo akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye pamoja na mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Mwanza Mwanza

Katika hotuba yake kwa wananchi wa jiji hilo, Lowassa aliwaahidi kushughulikia tatizo la usafiri wa maji kwa kununua meli mpya endapo watamchagua kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano.

“Najua moja ya matatizo ya hapa ni meli, mliahidiwa meli haijatolewa mpaka leo. Nawaahidi moja kati ya mambo nitakayoyafanya ni kuleta meli mpya,”alisema.

Suala la vijana kuhudhuria mafunzo ya JKT, Lowassa aliahidi kupendekeza idadi ya vijana wanaojiunga na JKT iongezeke mara nne ili vijana wengi wapate nafasi zaidi ya kushiriki katika mafunzo hayo.

“Lingine ni la JKT, JKT sasa hivi wanakwenda kwata mara moja kwa mwaka. Napendekeza JKT iongezwe mara nne, ichukue vijana mara nne ya sasa,” aliongeza.

Mwanza

Mgombea huyo wa Chadema alisisitiza kuwa serikali yake itaweka kipaumbele cha elimu kwa kuwa anaamini ukimuelimisha mtoto umempa hazina zaidi ya mali kama majengo.

Alisema kuwa elimu bure hadi chuo kikuu kwake inawezekana kwa kuwa zipo fedha nyingi zinapotea kutokana na misamaha ya kodi. Akitoa mfano, Lowassa alisema kuwa misamaha ya kodi nchini, hivi sasa inazidi bajeti ya kutoa elimu bure.

“Mwaka jana, serikali ilitoa msahama wa kodi wa shilingi Trilioni 1.8, hivi vitu ninavyosema hapa kwenye elimu vinagharimu shilingi Trilioni 1.3, kwa hiyo hela zipo,” alisema Lowassa ana kushangiliwa na umati huo.

Alitaja pia uwepo wa mali asili nyingi nchini ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kipato kinachoweza kulipia elimu bure.

Pia, aliahidi kilimo bora cha kisasa cha umwagiliaji, ambapo alieleza mfano wa nchi ya Misri ambapo alienda kuitembelea alipokuwa Waziri Wa Maji na kushudia vijana wanaomaliza chuo kikuu wakipewa mikopo na eneo la kufanya kilimo cha umwagiliaji kisha kuanza kulipa madeni hayo baada ya miaka mitano. Hivyo, alisema kuwa serikali yake itakuja mpango mkakati wenye mlengo huo.

Kingunge

Baada ya Kanda ya Ziwa, Lowassa anatajia kuingi katika mkoa wa Mbeya kuendelea na kampeni za lala salama, zikiwa zimebaki siku 11.

Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwasaidia watu waliopoteza fahamu kutokan na kukosa hewa kwenye msongamano

Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwasaidia watu waliopoteza fahamu kutokan na kukosa hewa kwenye msongamano, katika mkuano wa Lowassa, Mwanza

 

 

 

Jst Kidding: Young Dee asema Irene Uwoya ni Mpenzi Wake
Tanzia: Abdallah Kigoda Afariki Dunia