Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Luis Suarez, ameonyesha kipaji tofauti akiwa katika mazoezi ya timu ya taifa lake la Uruguay ambayo inajiandaa na mchezo kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Colombia.
Suarez alichukua jukumu la kukaa langoni mwa sehemu moja ya timu ya Colombia ilipokua ikifanya mazoezi na wakati mwingine alionyesha kuwa na utani mwingi dhidi ya wachezaji wenzake.
Mshambuliaji huyo mara nyingi amekua akicheza katika nafasi tofauti anapokua mazoezini lakini kitendo cha kukaa langoni, kimeonyesha kuwashughulisha waandishi wa habari waliokua wamefika kwenye mzoezi ya leo ya kikosi cha Uruguay.
Image: Suarez played as goalie in training with NT & collided with Godin. His teammates were worried about injury but he got back to normal. pic.twitter.com/ydGaI5uT6n
— Barcastuff (@barcastuff_real) October 11, 2016