Kundi la kigaidi la ISIS limewaua mashabiki takribani 14 wa Real Madrid waliokuwa wakiangalia mpira katika Makao Makuu ya chama cha mashabiki wa klabu hiyo kwenye mji wa Balad nchini Iraq, saa chache zilizopita.

Rais wa chama cha mashabiki hao aliyetajwa kwa jina la  Ziad Subhan amewaambia waandishi wa habari kuwa wanajeshi wa ISIS watatu waliingia katika jengo hilo wakiwa na silaha aina ya AK-47 na kufyatua risasi kwa watu waliokuwa ndani.

Alipoulizwa lengo la wanamgambo hao kuvamia makao makuu ya chama hicho cha mashabiki wa Real Madrid, alisema kuwa magaidi hao wanapinga mpira wa miguu.

Balad

“Hawapendi kabisa mpira wa miguu, wanadhani mchezo huu ni sehemu ya kupinga uislamu. Wanafanya mashambulizi kama hivi. Hili ni janga,” alisema Ziad Subhan.

Watu takribani 50 walikuwa wamekusanyika ndani ya ukumbi wa klabu hiyo wakiangalia mechi za nyuma za Real Madrid.

Damu zimeonekana zikitapakaa sakafuni huku picha za wachezaji wa timu hiyo pamoja na kocha wao, Zinedine Zidane zikiwa zinaninginia kutani.

 

 

AY, FA waivimbia Tigo Mahakama Kuu, Wapewa Tarehe ya kuvuna au kuchimba
Sumaye apata shavu, apenya kwenye 'moyo' wa Chadema

Comments

comments