Mchungaji wa kanisa la kiroho la Celestial Church of Christ (CCC) lililoko katika eneo la Abule-Egba jijini Lagos nchini Nigeria amemchoma moto muumini wake kwa madai kuwa alisikia sauti ya Mungu ikimuelekeza kufanya hivyo ili kuwahakikishia waumini kuwa yuko katikati yao na asingeungua.

Muumini huyo mwanamke aliyechomwa mkono wake aliyetajwa kwa jina moja tu la Bi. Bosede alieleza kuwa Mchungaji wao aliwaambiwa waumini kuwa amesikia sauti ya Mungu na kwamba imemwambia kuwa amchome moto muumini mmoja kati yao na kwamba asingeungua hata kidogo. Lengo likiwa kuwadhihirishia waumini hao kuwa yupo kati yao.

Achomwa moto

“Nilipotoka nje walinimwagia mafuta ya taa na kuniwashia moto. Ajabu nilianza kuungua kabla ya muumini mwingine kukimbilia moto, lakini kitendo hicho kilikuwa tayari kimeshafanyika,” alisimulia.

Mchungaji aliyetoa agizo hilo alipohojiwa na waandishi wa habari aliendelea kusisitiza kuwa ni kweli alisikia sauti ikimwambia amchome moto muumini na kwamba asingeungua.

“Niliisikia sauti vizuri kabisa. Lakini sijui nini kilitokea baada ya kuwasha moto juu ya mwili wake. Mungu amekuwa akiongea na mimi na imekuwa ikifanya kazi, kwahiyo ninashangaa kwanini sasa..” alisema Mchungaji huyo.

Mmoja kati ya waumini wa kanisa hilo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kuacha kusali katika kanisa hilo tena kwa sababu hawajui sauti ya ‘Roho Mtakatifu’ anayoisema Mchungaji huyo itamwambia amchome muumini gani siku za usoni.

Utafiti: Vijana wasema watampigia kura mgombea atakayewapa rushwa
Babu Tale amtetea Diamond kuhusu kauli hii kwa wasanii