Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi leo amefunga ndoa ya kifahari na mpenzi wake, Antonela Roccuzzo aliyekuwa rafiki yake wa utotoni.

Mrembo huyo alikutana na Messi kwa mara ya kwanza wakati mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka mitano tu nchini Argentina, kabla yajahamishiwa Uhispania akiwa na umri wa miaka 13 kujifunza mpira wa miguu.

Wawili hao wamefunga ndoa katika hotel ya kifahari kwenye jiji la Rosario, ikihudhuriwa na wageni 260, ikiwa ni pamoja na mastaa mbalimbali wa mpira wa miguu na tasnia nyingine.

Kati ya wageni walioshuhudia tukio hilo la kihistoria ni pamoja na wachezaji wenzake wa klabu ya Barcelona, Luis Suárez, Neymar, Gerard Piqué aliyeambatana na mkewe Shakira.

Vyombo vya habari vya Argentina vimeibatiza harusi hiyo jina la ‘Harusi ya Mwaka’ na vingine ‘Harusi ya Karne’.

Kamati ya utendaji ya TFF yakutana, yatoa maamuzi magumu kuhusu Malinzi
Utafiti: Kenyatta kumshinda Odinga uchaguzi Kenya