Washindi wa ‘Top 5 Miss Ilala 2018’ kwa kushirikiana na Dar24 Media wamefanya ziara mashuleni kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi wa kike kuhusu changamoto wanazokumbana nazo katika elimu.

Ziara hiyo imefanyika katika baadhi ya shule zilizopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuibua changamoto mbali mbali zinazorudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike katika elimu.

Hivyo, kufuatia ziara hiyo iliyoibua mambo mbali mbali katika elimu Dar24 pamoja na Miss hao wanaoenda kushirika mashindano ya Miss Dar es salaam 2018 na baadaye Miss Tanzania wameandaa kipindi kitakacho eleza kiundani changamoto za wananfunzi wa kike na nini kifanyike, lakini pia wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum, je Serikali inapaswa kufanya nini ili wanafunzi hao pia wafikie ndoto zao za kulitumikia Taifa.

Tazama hapa matukio katika picha, na kipindi kitarushwa Julai 27, 2018 kupitia Dar24 TV na katika tovuti hii.

 

 

Imran Khan aongoza kura za uchaguzi mkuu
Pompeo amkingia kifua Rais Trump

Comments

comments