Upepo wa mahaba ya Rihanna bado unalipuliza jicho la Chris Brown ingawa wawili hao walipigana chini kwa kishindo mwaka 2009, baada ya Breezy kumshushia mrembo huyo kipigo kilicholaaniwa na kila anayethamini utu.

Picha mpya za Rihanna akiwa kwenye mavazi ya ufukweni akiwa anasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa ya msusi wake, Yusef Williams zilizowekwa mtandaoni na mtu wao wa karibu Agosti 9 mwaka huu, zimedaiwa kumchanganya tena Chris.

Katika picha hizo, RiRi mwenye umri wa miaka 30 anaonekana akiwa mwenye umbo zuri jembamba lililokubali mazoezi na kumrejeshea mvuto wa ‘ujanani’, tofauti na picha za mwisho zilizokuwa zikimuonesha amenenepa na kuweka hatarini umbo lake matata.

Chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa Chris, amenukuliwa na Hollywood Life akieleza kuwa Chris ameonesha wazi kuvutiwa na muonekano mpya wa Rihanna.

“Chris anadhani Rihanna anamuonekano mzuri wakati wote, lakini alipoziona hizi picha alivuta umakini zaidi na zilimchanganya. Ana muonekano mzuri zaidi hivi sasa na ni muonekano halisi. Hicho ndicho Chris aanapenda zaidi, ni mwanamke mwenye muonekano halisi,” chanzo hicho kimenukuliwa.

Moto wa uzuri wa Rihanna umeonekana tena mwaka huu alipofunika jarida la Vogue la Uingereza, toleo la Septemba mwaka huu. Septemba ndilo huwa toleo lenye mvuto zaidi na lenye nguvu.

Rihanna na Chris Brown wana historia ya aina yake kwenye uhusiano wao ambao ulizimwa mwaka 2009 baada ya Chris kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kumpiga vibaya usoni mrembo huyo. Alipewa adhabu baada ya kukutwa na hatia.

Hata hivyo, baadaye Rihanna alirudi kumsaidia Chris na hata kuhudhuria kesi dhidi yake akiwa ubavuni mwake. Uhusiano wao ulileta shida zaidi baada ya Chris kuwa na uhusiano pia na mrembo Karruache Tran na kumfanya kuwa katika njia-panda ya uhusiano na warembo hao.

Tangu wakati huo, Rihanna na Chris wamekuwa na urafiki na uhusiano unaowaka na kuzima, lakini hivi sasa kila mmoja ‘anacheza na hamsini zake’.

AY na mkewe wapata mtoto wa kiume, ataja jina na maana yake
Kamwelwe akazia ving'amuzi kufuata sheria, Clouds TV, ITV zaondolewa

Comments

comments