Ruqia Hassan, mwanamke mrembo mwenye umri wa miaka 30 ameuawa kikatili kwa kukatwa kichwa na kundi la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Syria (ISIS) baada ya kulipinga wazi

Mwanamke huyo ambaye ni mwanaharakati ambaye alikuwa anaishi Raqqa ambapo ni ngome nyingine ya ISIS, ameripotiwa kuwa aliuawa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.

Kundi la ISIS liliifahamisha familia ya mwanamke huyo wiki hii huku likiieleza kuwa aliuwa baada ya kubainika kuwa alikuwa analipeleleza kundi hilo kama msaliti.

Kwa mujibu wa CNN, Bi. Hassan alikuwa mmoja kati ya wanawake wachache wa jiji hilo waliokuwa wakitafuta namna ya kuiambia dunia kuhusu kile kilichokuwa kikifanyika katika jiji hilo.

 

Waliovamia shamba la Sumaye watimuliwa
Mahakama Yaweka Zuio la Muda Bomoabomoa, Ni kwa Nyumba Hizi Pekee