Mnamo Julai 1, 2018 Rais John Pombe Magufuli alimteua Mbunge wa Mwibara na aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingura, Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.

Leo Jumanne Julai 10, 2018 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba rasmi amekabidhi ofisi hiyo kwa Waziri mpya, Kangi Lugola ambaye tayari alikwishaanza kazi mara baada ya uteuzi huo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mwigulu ambaye kwa sasa amebakia kama Mbunge wa Iramba Magharibi ameandika.

“Makabidhiano ya ofisi/kijiti hii leo Dodoma. Namtakia kila la kheri Mh. Kangi Lugola katika utumishi wake kwa watanzania katika wizara hii”.

Aidha Mwigulu Nchemba mara baada ya kuenguliwa nafasi hiyo alifika jimboni kwake na kuongea na wanachi wake akisema kuwa sasa atapa nafasi ya kuwatumikia vyema wananchi wake.

 

 

Video: Alichoongea Mwigulu baada ya kukabidhi ofisi kwa Lugola
Kenedy kupimwa afya leo