Nicki Minaj amekabidhiwa rasmi ufunguo wa Queens ambayo iko ndani ya jiji la New York nchini Marekani.

Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Onika Tanya Maraj alipewa ufunguo huo na rais wa Queens, mwanasiasa nguli wa kike, Melinda Katz kutokana na jinsi alivyofanikiwa katika sanaa ya muziki.

Mkali huyo wa ‘Anaconda’ alitumia Instagram kuelezea furaha yake na kupost picha ya funguo ya dhahabu aliyopewa na kiongozi huyo wa Queens.

“what a pleasant surprise? Wish I was there to receive it. Thank you so much! #MelindaKatz hopefully we can meet b4 I fly out again #NewYork #Queens.” Ameandika.


Nicki alikutana na zawadi hiyo akiwa jijini New York kwa ajili ya tuzo za NBA zinazoongozwa na NBA. Rapa huyo alitumbuiza katika tuzo hizo.

Video: Maalim Seif afunguka makubwa, aitwika zigo la lawama RITA
Wakenya hatarini miaka 5 Jela kwa lugha chafu mtandaoni wakati wa uchaguzi