Rapa kala Jeremiah na Roma Mkatoliki mepema leo walikuwa wakichota busara za Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa walipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wasanii hao, walifanya mazungumzo na Lowassa leo asubuhi ingawa hawakueleza walichozungumza na mwanasiasa huyo mkongwe aliyegombea urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa.

“VIJANA WANAPOKUTANA NA MZEE. #MUNGUIBARIKITANZANIA,” ameandika Kala Jeremiah kwenye picha waliopoz na Lowassa.

Roma na Lowassa 22

Naye Roma Mkatoliki ambaye muda mfupi ujao ataachia rasmi wimbo wake mpya ‘Kaa Tayari’ aliowashirikisha Jos Mtambo na Darassa, amepost picha kaka hiyo na kuandika “MAPEMA LEO ASUBUHI!! #DoneTheMeeting With Hon. #E_LOWASA  Bado Masaa Machache Niachie Ngoma Yangu Mpya Leo.

Roma na Lowassa

Ubalozi wa Uingereza wampa Shavu Diamond Platinumz
ICC Kuzishtaki Uganda na Djibouti kwa Kutomkata Bashir