Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameamua kuionesha dunia anachojivunia kama baraka kutoka kwa Mungu, akiwa na wanae watatu.

Ronaldo ameweka kwenye akaunti yake ya Instagram picha inayomuonesha akiwa na watoto wake mapacha aliowapata hivi karibuni, pamoja na mtoto wake mwenye umri wa miaka 7, Cristiano Jr.

Mchezaji huyo na mwanaye wanaonekana wakiwa wenye furaha wakiwabeba watoto wapya huku wakipeana tabasabu bashasha.

Huenda Ronaldo akawa amembeba mtoto wa kiume aliyemuita Mateo, na mwanae Cristiano amembeba mdogo wake aliyepewa jina la Eva.

Blessed

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on


CR7 alitangaza taarifa za kuwapata watoto wake mapacha kupitia mtandao wa Facebook akiambatanisha picha inayomuonesha akiwa amewabeba na ujumbe uliosomeka, “nina furaha sana kuweza kuwabeba watoto hawa mapacha ambao ni wapendwa wa maisha yangu.”

Mshindi tuzo ya Uingereza afika bungeni
JPM: Sisafiri sasa hivi, lazima niwanyooshe kwanza, hizi safari zipo tu