Kikosi cha Klabu ya SSC Napoli ya Italia usiku ya jana jumanne (Januari 17) kilivaa jezi toleo maalum kwa ajili ya sikukuu ya wapendanao (Valentine Day 2023).

Jezi hizo zimevaliwa katika mchezo wa Coppa Italia, ambao ulimalizika kwa SSC Napoli kupokea kichapo cha penati 5-4 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 2-2 dhidi ya Cremonese.

Mapato yatokanayo na mauzo ya jezi hizo, yataenda kusaidia mashirika ya misaada ya ukatili wa kijinsia.

Gwajima azindua mradi uimarishaji afya mazingira hatarishi
Mnyeti, Clouds FM waishika pabaya TFF