Kikosi cha Taifa Stars kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

Stars ilianza kambi Machi 8 jijini Dar es salaam huku ikifanya mazoezi Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo moja ya mchezaji ambaye yupo kwenye maandalizi hayo hayo ni mkongwe Kelvin Yondani.

Kocha Kim Poulsen aliita kikosi cha wachezaji 40, kwa ajili ya kujiandaa na michezo dhidi ya Libya na Equatorial Guinea, ambayo itatanguliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kenya.

Paulsen amesema anaamini kikosi kinachoendelea na maandalizi ya michezo hiyo, kitafanya vizuri, huku akiwataka watanzani kutoa ushirikiano kwa timu yao ya Taifa Stars.

“Wachezaji tutakuwa nao na kila mmoja atafanya kazi kwa kutimiza majukumu yake uwanjani, kila kitu kitakuwa sawa hivyo mashabiki watupe sapoti.”amesema kocha huyo kutoka nchini Denmark.

Msolla awakingia kifua GSM
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 10, 2021