Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeondoka nchini kuelekea Cameroon tayari kwa fainali za Mataifa Bingwa ya Afrika zitakazofanyika nchini Cameroon kuanzi Januari 16.

Taifa Stars mapema leo alfajiri ilianza safari ya kuelekea kwenye fainali za CHAN katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKNIA).

Kabla ya kuanza safari ya Cameroon, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega alikabidhi bendera kwa Kikosi cha Taifa Stars ambacho kimepangwa kundi D lenye timu za Zambia, Namibia na Guinea, na michezoya kundi hili itachezwa mjini Limbe.

 Taifa Stars itaanza kusaka taji la Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN) kwa kucheza dhidi ya Zambia Januari 19 kwenye Uwanja wa Limbe, kicha itarejea tena dimbani Januari 23 kupepetana na Namibia na itamaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kukutana dhidi ya Guinea Januari 27.

Jafo aagiza Mkurugenzi kusimamishwa kazi
Young Africans wafichua siri ya kuidhibiti Simba SC