Hatimaye mmoja kati ya wasanii wa kike wakongwe kwenye muziki wa rap duniani, MC Lyte hatimaye amepata mwenza na kufunga nae ndoa mwishoni mwa wiki huko Montego Bay, Jamaica.

Lyte mwenye umri wa miaka 46, amefunga pingu za maisha na mwanajeshi mstaafu John Wyche ambaye wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

Akizungumza na jarida la Essence, Lyte amesema ilikuwa ni sherehe nzuri na ana furaha kupata mfalme wake.

Kwa upande wa mumewe, Wyche amesema ilikuwa kumbukumbu nzuri kuona watu wengi wakihudhuria ndoa yao huku akielezea mwanzo wa safari yao ya mahaba.

“Tulianza na mwanzo mzuri, miezi michache baada ya kumjua Lana [MC Lyte] nilijua huyu ndiye mwanamke ninayemhitaji kuwa mke wangu,’’ amesema Wyche.

Sherehe za ndoa hiyo zilifanyika katika fukwe za Jamaica na kuhudhuriwa na wasanii wengi akiwemo Lil Mama, muimbaji wa SWV Coko na Kelly Prince.

Lyte na mumewe walikutana Machi 2016. Wyche alimvisha Lyte pete ya uchumba mapema mwaka huu.

Horn ataka Manny Pacquiao apimwe mkojo bila mpangilio
Mkongwe Wa Ligi Ya England Kuhamia The Hawthorns