Mzee mmoja wa makamo amevunja mitandao kwa picha yake hivi karibuni kwa kile alichoamua kikifanya katikati ya show kubwa ya Beyonce wakati mashabiki wakichanganyikiwa na utumbuizaji wa mwimbaji huyo huko kusini mwa Carolina.

Mzee huyo alionekana akiwa amekaa kuelekea upande wa jukwaa, lakini pamoja na kwamba Beyonce aliangusha show kali kama kawaida, mzee huyo alikuwa bize akisoma kitabu chake kwa muda mrefu tu.

Mzee

Mashuhuda walieleza kuwa mzee huyo alipelekwa kwenye tamasha hilo na mkewe ambaye ni shabiki mkubwa wa Beyonce lakini kilichokuwa kukifanyika kwake kilikuwa kinampotezea muda tu.

Chanzo cha ABC kilizungumza na mzee huyo kutaka kujua kulikoni anajisomea katikati ya show kubwa ya Beyonce wakati mashabiki wengine wakipiga shagwe kubwa.

Mzee huyo alimueleza kuwa yeye hakuvutiwa na show hiyo kwa sababu aina ya miziki iliyokuwa inapigwa sio aipendayo.

“Niliona show ya Beyonce nzuri na inavutia, lakini muziki wake…uko sawa lakini sio mtindo wangu. Mimi husikiliza miziki ya miaka ya 1950, 1960 na 1970 na miziki mingi ya Kigiriki,” alisema.

Julio Azipa Ushauri Wa Bure Simba, Young Africans
Msichana wa miaka 9 aliyeokolewa mikononi mwa Boko Haram agoma kula, ataka arudishwe akaishi na ‘mumewe’