Wakati pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani likifunguliwa, baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa mstari wa mbele kuchukua fomu hizo wakiwepo mawaziri.

Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fredrick Lowassa amechua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha mapinduzi (CCM) ya kugombea ubunge jimbo la Momnduli.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo, leo Jumanne Julai 14, akimkabidhi Fredrick Lowassa

Waziri wa Uwekezaji, Angela Kairuki amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Same Magharibi.

Waziri wa Uwekezaji Kairuki akikabidhiwa fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi leo Julai 14 , 2020.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima achukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambalo lilikuwa chini ya Halima Mdee wa CHADEMA.

Gwajima akichukua fomu leo.

Dkt. Tulia Ackson amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Dkt. Tulia akilipa fedha ya kuchukulia fomu leo.

Mrisho Gambo achukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Gambo akionesha fomu baada ya kuichukua leo.

Wengine waliochukua ni Mlinzi wa zamani wa Baba wa Taifa, Aloyce Tendewa ambaye amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kilombero, Francis Nanai, Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe.

RC mstaafu Mwanri achukua fomu jimbo la Siha
Ambani ashtushwa na kipigo cha Simba SC