Kundi la wakimbizi kutoka Iran waliokwamba katikati ya mpaka wa Ugiriki na Macedonia kwa takribani siku nne wamejishona midomo yao kwa nyuzi na sindano kupinga kuzuiwa kuvuka mpaka. Wakimbizi hao wanaotaka kuelekea Ulaya Magharibi wamechukua uamuzi huo kama sehemu ya kushawishi Mecedonia kuwafungulia mpaka huku wakieleza kuwa hawawezi kurudi Iran kwa kuwa watanyongwa huko endapo watafanya hivyo. Wakimbizi Iran 2 Tangazo la kufunga mipaka linatekelezwa kutokana na shambulizi la kigaidi la Novemba 13 lililochukua uhai wa watu zaidi ya 300 katika jiji la Paris nchini Ufaransa.   Mmoja kati ya wakimbizi hao aliyehojiwa alieleza kuwa yeye ni fundi mzuri wa masuala ya umeme hivyo atakuwa sehemu ya uzalishaji katika nchi yoyote atakayoingia na sio vinginevyo.

Rais Kenyatta Awapiga Chini Mawaziri Wote Wenye Kashfa Za Ufisadi
Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi La Polisi Mwanza Kuhusu Kesi Ya Mawazo