Kanye West ameendelea kushika vichwa vya habari kila kukicha. Muda mfupi baada ya kuvuma kwa taarifa zake kuhusu birthday part ya binti yake mdogo North West, na mambo kadhaa ya kimahusiano ya kumuhusisha yeye na anayetajwa kuwa mpenzi wake mpya Muigizaji Julia Fox na habari zake za kutengana na mzazi mwenzie mrembo Kim Kardashian.

Jipya limezuka kumuhusu rapa huyo, na hili ni kutoka Shirika la kutetea haki za wanyama la nchini Marekani ‘PETA’ ambalo limetoa taarifa ya kuchukizwa na kitendo cha rapa Kanye West kutumia picha ya nyani aliyechunwa kama Cover kaajili ya wimbo wake mpya alioshirikiana na rapa The Game.

Muda mfupi baada ya Kanye kuzindua wimbo wake mpya “Eazy” akishirikiana na The Game, shirika hilo la kutetea haki za wanyama kupitia kwa Rais wake, lilitoa taarifa likiwashutumu wawili hao kwa kutumtumia nyani aliyechunwa ngozi katika sanaa yao kwa madai ya kuwa si jambo la Kibinadamu.

Kwa mujibu wa Billboard Rais wa ‘PETA’ Ingrid Newkirk, alisema kuwa  “Picha hiyo inamkumbusha nyani ambao PETA imewapata, wakati mwingine vichwa, wakati mwingine mikono, wakati mwingine mwili mzima, katika soko la nyama duniani kote,”

“hii inaweka wazi kuwa unapoondoa manyoya huwezi kukosa kwamba kuna mtu ndani, ni nyani wenzetu, na si wa kuwanyanyasa  kwa malengo yoyote, si maabara, mbuga za wanyama za barabarani, sinema, au soko la nyama.” alisema.

Mpaka sasa hakuna yeyote kati ya Kanye na The Game aliyejibu tuhuma hizo licha ya picha hiyo kuendelea kuwepo kwenye kurasa zao za mitandao yao ya kijamii kama tangazo la wimbo wao mpya ‘Eazy’.

Kanye na Game wamewahi kufanya kazi kadhaa wakiwa pamoja ikiwamo ‘Wouldn’t Get Far’ mwaka 2006 pamoja na  ‘Dreams’ kutoka kwenye album ya kwanza ya The game aliyoiachia mwaka 2005.

Ratiba ya 32 bora ASFC hadharani
Wanne washikiliwa kwa kula nyama za watu