Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans mapema leo Jumanne (Novemba 29) majira ya asubuhi kimeondoka jijini Mbeya kuelekea mjini Mbarari, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao Ihefu FC.

Mchezo huo uliopangwa kuanza kuunguruma mishale ya saa kumi jioni, utapigwa katika Uwanja wa Highlands Estates, uliopo mjini Mbarari.

Katika mchezo huo Young Africans itakua na kazi ya kuendeleza Rekodi yake ya kucheza mchezo wa 50 bila kupoteza, ili hali wenyeji wao Ihefu FC watahitaji kuivunja Rekodi hiyo na kupata alama tatu muhimu.

Picha: Waziri Mkuu kassim Majaliwa akikagua mradi wa maji Kisarawe
Moses Phiri: Naweza kuwa mfungaji bora