Kikosi cha Young Africans kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Kagera, tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 dhidi ya Kagera Sugar.

Young Africans wamesafiri kwa ndege leo asubuhi, huku wakiwa na sura za furaha kufuatia kuwafunga watani zao wa jadi Simba SC bao 1-0, na kutwaa Ngao ya Jamii Jumamosi (Septamba 25).

Mabingwa hao wa kihistoria watakua ugenini Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera keshokutwa Jumatano, kuikabili Kagera Sugar ambayo itakua nyumbani.

Mchezo huo unatarajiwa na upinznai mkubwa hasa ikizingatiwa kwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana uwanjani hapo, Young Africans ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mukoko Tonombe, huku mchezo wa mzunguuko wa pili uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa timu hizo zilifungana mabao 3-3.

Kaze: Nimekuja kuipa mataji Young Africans
Makamba: TANESCO iendeshwe kibiashara