Rapa Young Dee amesema kuwa anajuta kupiga picha ‘tata’ zisizozingatia maadili ya Kitanzania na mwimbaji Amber Lulu kwani zilimsababishia matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kukosana na mama yake mzazi.

Young Dee ambaye hivi karibuni ameutambulisha wimbo wake mpya ‘Kiutani Utani’ amesema kuwa picha hizo zimemuumiza na kwamba ametumia muda mwingi kurudisha uhusiano wake mzuri na mama yake.

“Ile picha iliniumiza mimi sana-sana. Mimi I didn’t see it coming (sikuona kama inakuja kuwa vile). Nilimuelewesha mama kwa kutumia njia nyingine ili aone sio big deal (sio kitu kikubwa/cha maana),” Young Dee alifunguka katika mahojiano na 100.5 Times FM. “Tatizo watu wengine ndio imekuwa vigumu kuelewa,” aliongeza.

Paka Rapa amesisitiza kuwa anahisi Amber lulu ndiye aliyesambaza picha hizo zilizosababisa pia wote wawili kuhojiwa na jeshi la polisi.

Wawili hao waliwahi kuwa katika uhusiano wa mapenzi ambao ulivunjika, huku kila mmoja akimtupia mwenzake lawama za ‘utoto’.

Ray C aizunguka Afrika Mashariki kuwasaka watu wake
LIVE KENYA: Mahakama Kuu ikitoa sababu za kufutwa matokeo ya Urais, "Madai ya udukuzi yalikuwa ya kweli"