Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya ziara yake maalum ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika ziara hiyo, Rais Shein amepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani.

DSC_9092

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakati alipowasili katika Ufunguzi wa Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

DSC_9106

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kufungua  Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

DSC_9278

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akipokea risala ya Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Abdalla (Mabodi) baada ya kulifungua rasmi Tawi hilo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

DSC_9407

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali na Wananchi wa Chama cha Mapinduzi wakati wa ufunguzi wa Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

DSC_9686

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akiwasalimia Watoto wa maeneo ya Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la CCM  la Muembe Matarumbeta  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

DSC_9691

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akiwapungia mkono wanachama wa CCM na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la CCM la Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika kwa shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la hilo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,

Video: Vilio, simanzi vyatawala shule ya Lucky Vicent
Rais Shein awashukia mawaziri, ‘mnachokitafuta mtakipata’