Mtendaji mkuu wa klabu ya Inter Milan Piero Ausilio, ametetea maamuzi ya kutimuliwa kwa eliyakua meneja wa kikosi cha klabu hiyo Frank de Boer.

Ausilio, alizungumza na waandishi wa habari mjini Milan na kueleza kuwa, Inter Milan ilifanya makosa ya kumpa ajira Frank de Boer, kutokana na mazingira ya haraka yaliyokua yanawakabili mwanzoni mwa msimu huu.

Ausilio, amesema walibaini wamekosea kufanya maamuzi hayo, kutokana na uhalisia wa meneja huyo kutoka nchini Uholanzi kukosa uzoefu na ligi ya nchini Italia, lakini walijiaminisha huenda angeweza kufanya maajabu, jambo ambalo lilishindikana.

Amesema siku zilivyokua zinasogea ndipo walijiridhisha kwamba, Frank de Boer hatoweza kuhimili mikiki mikiki ya ligi ya nchini Italia na ndipo walipoanza kukaa vikao na kumjadili, na hatimae mwanzoni mwa juma hili walitangaza kumtimua.

Frank de Boer alitimuliwa klabuni hapo baada ya kuitumikia ajira yake kwa siku 85 pekee, na alikishuhudia kikosi cha Inter Milan kikicheza michezo 11 ya ligi huku kikishinda michezo minne, kufungwa michezo 5 na sare mara mbili.

Kwa sasa kikosi cha Inter Milan kimekabidhiwa kwa aliyekua kocha wa kokosi cha kwanza Stefano Vecchi, ambaye usiku wa kuamkia hii leo alikua katika benchi la ufundi kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Europa league dhidi ya Southampton ambao wamechomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Magufuli ajibu madai ya kukandamiza demokrasia, Udikteta
Wakala Wa Yaya Toure Kuzungumza Na Pep Guardiola