Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Fatma Karume amesema kuwa Watanzania wamemtetea Piere kwakuwa ni haki ya binadamu kuishi maisha anayoyataka yeye, na wanaombeza wanakosea.

Karume amesema kuwa, anachokifanya mchekeshaji huyo ni sahihi na havunji sheria za nchi hivyo ni haki yake ya msingi kuishi anavyotaka kwakuwa hamkwazi mtu katika maisha yake.

“Pierre mimi nimechelewa kumjua kwani sijamjua mapema hadi pale alipoitwa wa hovyo hovyo, hii sio haki ni kumkosea mtu haki yake ya msingi, hakuna mtu wa hovyo hapa duniani,” amesema Karume.

Akizungumzia namna Piere alivyoambiwa kuwa ni moja kati ya watu wa hovyo, amesema kuwa anatakiwa kumshukuru Makonda kwakuwa amefanikiwa kumpiga teke chura lililomuongezea hatua kubwa.

Aidha, hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa ‘hovyo’ kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.

Hata hivyo, Miongoni mwa kauli hizo, Makonda alisema,”Wakina mama kama hawa wanaojituma na kuhangaika kwa ajili ya watoto, wao ndio tuwape kipaumbele, sio hawa walevi walevi, yaani unakuwa na taifa ambalo watu wa hovyo ndio wanakuwa maarufu”.

  • Lema azungumza baada ya kuadhibiwa, awapa ujumbe wabunge
  • JPM amfagilia Mkapa, bila yeye nisingekuwa waziri au Rais
  • RC Mtaka azindua kambi za kitaaluma mkoani Simiyu

Vodeo: Lema kifungoni hadi mwaka 2020, Uchaguzi serikali za Mitaa Oktoba
Makala: Nipsey Hussle, 'damu ya Afrika’ iliyotikisa Marekani, kumshika Jay Z na kuuawa