Klabu ya Borussia Dortmund imethibitisha kuwa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang ameondoka klabuni hapo na muda mfupi baadaye

picha ya mchezaji huyo akiwa amevaa jezi ya Arsenal ikaonekana ikiwa inasambaa kwa kasi.

Aubameyang anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa gharama kubwa kikosini hapo, kwani amesajiliwa kwa pauni milioni 56 huku mshahara wake ukiwa ni pauni 180,000 kwa wiki.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 28 inadaiwa kuwa ni sehemu ya dili la straika wa Arsenal, Olivier Giroud kuondoka klabuni hapo kwenda Chelsea huku ikielezwa kuwa straika wa Chelsea, Michy Batshuayi akiwa njiani kwenda Dortmund.

Kamati ya maadili yamtupa jela Edger Chibula
Mengi aipa TWCC jengo lake kuendeleza ujasiriamali