Serikali kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi wamekubaliana kutumia mbinu za kisasa na za jadi ikiwamo matumizi ya pilipili kuwadhibiti tembo na wanyamapori wengine wanaovamia makazi ya watu na mashamba kwenye vijiji vinavyopakana na hifadhi.

Akizungumza jijini Mwanza juzi wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili madhara ya wanyama pori kwa binadamu na mbinu ya kukabiliana nayo, Naibu katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii, Dk Aloyce Nzuki amesema mpango huo ni mkakati wa kitaifa.

mashamba ya pilipili kama uzio kuzunguka vijiji na nyumba za wakazi maeneo yanayopakana na hifandhi.

“Huu utakuwa ni mkakati wa kitaifa katika malengo ya muda mfupi, kati na mrefu na kudhibiti muingiliano kati ya wanyama pori na binadamu” amesema Dkt. Nzuki.

Mikakati hii inakuja huku kukiwa na taarifa za watu 96 kuuawa na wengine 90 kujeruhiwa kutokana na matukio ya uvamizi wa wanyamapori yaliyotokea kati ya mwaka 2018/19.

Hali kadharika katika kipindi cha mwaka 2015 na 2019, zaidi ya eka 14,000 za mazao ziliharibiwa na wanyamapori waliovamia mashamba ya wakulima nchini.

Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha amesema licha ya mashamba ya pilipili njia nyingine itakayotumika kuwadhibiti wanyamapori ni ufugaji wa nyuki maeneo ya mipaka ya vijiji na hifadhi.

“Matumizi ya pilipili na nyuki kudhibiti uvamizi wa wanyamapori tayari yameanza maeneo ya iringa karibu na hifandi ya Udzungwa” amebainisha Dkt. Msuha.

Ofisa wanyamapori wilaya ya Meatu, Revocatus Meney amebainisha njia nyingine ni kuwa wananchi wanaopakana na hifadhi kutolima mazao yanayopendwa na wanyamapori.

Wanaume wenye michepuko hatarini kupata tezi dume
Serikali yabainisha idadi ya familia zilizotaka vipimo vya DNA kuhakiki Baba