Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni muumini wa filosofia ya amani na utulivu katika harakati za kuleta maendeleo zaidi nchini kupitia mabadiliko ya uongozi yanayotarajiwa baada ya mwezi Octoba, 2015.

Akitoa hutuba wakati akifunga sherehe za wiki ya serikali za mitaa mjini Mtwara, Pinda amewaonya wanasiasa wafitini na wanaotengeneza chuki miongoni mwa jamii maarufu kama ‘wazee wa fitina’kutosababisha machafuko na fujo kwa wale watakaokuwa wametangazwa kuwa washindi katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini.

“Acheni kuweka chuki zisizo na tija, haitasaidia,” alisema. “Acheni kutaka kuwafanyia fujo wale watakaoukuwa wamekubalika katika ngazi mbalimbali kutuongoza. Maana wengine kazi yao ni fitina tu na wanataka mambo yaende hovyo.”

Mizengo Pinda ambaye pia ni mmoja kati ya wagombea waliorudisha fomu za kuwania kuteuliwa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM aliwataka wanasiasa wenzake kukubali matokeo yoyote na kummunga mkono atakayechaguliwa na ngazi husika za chama.
“Mzalendo wa kweli ni Yule anaekubali. Kama kura hazikutosha hazikutosha tu,” alisema Pinda.

Luis Nani Kucheza Soka Uturuki
Video Mpya: Love Boat - Kcee feat. Diamond Platnumz