Nyota wa muziki wa Singeli, Dulla Makabila ameitwa na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, kwa ajili ya majadiliano kuhusu wimbo wake mpya ‘Pita huku’ aliouachia siku chache zilizopita.

Makabila, ameitwa kupitia barua iliyotoka kwa katibu mtendaji wa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana ikieleza kuwa, “Basata inapenda kuwajulisha kwamba kutakuwa na kikao kitakachofanyika tarehe 21-12-2022 siku ya jumatano, ajenda ya kikao ni kujadili kuhusiana na wimbo wako mpya ‘Pita huku’.

Dulla Makabila.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Makabila amethibitisha kuipokea barua hiyo ya wito kwa kuandika ujumbe mfupi wa kuitikia wito huo.

Andiko hilo linaeleza kuwa, “Mashabiki zangu Asanteni Kwa kuufanya wimbo wetu wa ‘pita huku’ kuwa trending number moja huko Mjini Youtube, tuendelee kufuatilia kazi nzuri.”

Rufaa ya Sabaya kusikilizwa desemba 28, 2022
Wazazi wakutana kwa Mfalme Mohamed VI