Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Al Ahly wametamba kuishambaratisha Simba SC, kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi A, kesho Jumanne (Februari 23) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tambo za Al Ahly zimetolewa na kocha mkuu wa klabu hiyo yenye mskani yake makuu mjini Cairo, Misri Pitso Mosimane alipozungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam.

Mosimane amesema amekiandaa vyema kikosi chake kuelekea mchezo huo, hivyo hana shaka na wapinzani wao Simba SC, licha ya kuwa nyumbani kwao.

“Tupo tayari kwa mchezo na hakuna la kuhofia. Muda wa mchezo wetu si sababu ya kubadili kikosi, tupo tayari kwa mapambano.”  amesema kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

Al Ahly waliwasili Dar es salaam mapema Jumamosi (Februari 20), na wamekua wakifanya mazoezi yao Uwanja wa Gymkhana, huku hali ya hewa ya jiji la Dar e salaam ikitajwa kuwa kikwazo kwao.

Kwa sasa jijini Dar es salaam kuna joto kali, na tetesi zilieleza kuwa huenda kocha huyo akapanga kikosi tofauti kutokana na changamoto ya hali ya hewa waliyokutana nayo, lakini amekanusha alipoulizwa hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari hii leo.

Al Ahly wanaongoza msimamo wa Kundi A kwa kuwa na alama tatu, kufuatia ushindi wa mabao matatu dhidi ya Al Mereikh ya Sudan, huku SImba SC ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo kwa kuwa na alama tatu, baada ya kuwafunga AS Vita Club bao moja kwa sifuri.

Wanne washikiliwa tuhuma za uvamizi Bunge la Marekani
Simba SC: Tutaikalisha Al Ahly kwa Mkapa