Rais wa shirikisho la soka la Ulaya ambaye amesimamishwa Michel Platini amesema hatawania urais wa Fifa mwezi ujao.

Platini, pamoja na rais wa FIFA, Sepp Blatter, wamepigwa marufuku kutojihusisha na shughuli za soka kwa miaka minane na shirikisho hilo linalosimamia soka duniani.

Wawili hao walipatikana na makosa ya ulaji rushwa kuhusiana na malipo ya £1.3m ($2m) yaliyopewa Platini mwaka 2011.

Wamekata rufaa dhidi ya marufuku hizo, lakini Platini anasema hali kwamba uchaguzi unafanyika tarehe 26 Februari ina maana kwamba hawezi akawania.

“Nimejiondoa kutoka kinyang’anyiro cha kuwa rais wa Fifa,” Mfaransa huyo wa umri wa miaka 60 ameambia shirika la habari la Associated Press.

“Sina mbinu na uwezo wa kushindana na wagombea wengine kwa usawa. Sijapewa muda wa kushiriki kwenye ‘mchezo huu’ kwa usawa na wengine. Kwaheri Fifa, kwaheri urais wa FIFA.”

Waliobaki katika kinyang’anyiro cha uraisi wa FIFA.

  • Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa – 50, Bahrain
  • Tokyo Sexwale – 62, Afrika Kusini
  • Prince Ali bin al-Hussein– 40, Jordan
  • Gianni Infantino – 45, Uswizi
  • Jerome Champagne – 57, Ufaransa

Audio: Wastara Alia na Ushiriki wake kwenye Kampeni na Kinachotokea kwenye Bomoabomoa
Oscar: Sina Mikwaruzano Na Diego Costa