Wajumbe wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, jana walikutana kwenye makao ya shirikisho hilo huko mjini Nyon nchini Usiwz kwa lengo la kutafuta namna ya kumuunga mkono rais Michel Platini katika harakati za kuwania kiti cha uongozi FIFA.

Wajumbe wa shirikisho hilo bado wanaamini Platini, ana nafasi ya kipekee kuwania kiti cha urais wa FIFA, licha ya kukabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa siku tisini, kwa ajili ya kupisha uchunguzi ya ubadhuilifu wa fedha.

Tayari baadhi ya mataifa ya barani humo, yameshaweka wazi mpango wa kumuunga mkono Platini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa urais wa FIFA, kwa kuamini mpaka sasa kiongozi huyo hana hatia.

 

Viongozi wa chama cha soka nchini England FA, walikua mstari wa mbele kuongoza kampeni hiyo siku moja baada ya kamati ya maadili ya FIFA kutangaza adhabu kwa Platini pamoja na wenziwe watatu.

 

Hata hivyo mpaka sasa, muafaka wa kuungwa mkono kwa Platini katika harakati za kuwania kiti cha urais wa FIFA haujapatikana kutokana na baadhi ya wajumbe kutoka mataifa ya barani Ulaya kushindwa kutangaza msimamo wao.

 

Hii leo mkutano wa wajumbe kutoka nchi 52 ambao ni wanachama wa UEFA, unatarajiwa kutoka na jibu moja la kukubaliana na azimio la kumuunga mkono kiongozi wao ama kumkataa.

 

Katika hatua nyingine mkutano huo utafanya uamuzi wa kupitia maazimio yaliyopitishwa juma lililopita la kumtaka Platini aheshimu maamuzi ya kufungiwa kwa siku 90, kwa kuiachia nafasi ya urais wa UEFA.

 

Klopp: Nimebaini Jambo Kikosini
Raul Atangaza Kustaafu Soka