Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini amesema bado ana moyo wa kutaka kumrithi Sepp Blatter katika kiti cha urais wa FIFA, kupitia uchaguzi uliopangwa kufanyika februari 26 mwaka 2016.

Platini, amejionadi kuendelea kuwa katika matamanio ya kuhitaji kuiongoza FIFA kama rais, huku akiendelea kukanusha kuhusika na ufusadi uliojikita ndani ya shirikisho hilo kwa jina lake kuhusika.

Platini amekuwa rais wa UEFA tangu mwaka 2007, na alipewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa FIFA kabla ya sakata hilo kuibuliwa na serikali ya nchini Uswis, na sasa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya mataifa ya barani Ulaya kutokumuunga mkono kutokana na tuhuma zinazomkabili.

Jackson Mayanja Atimuliwa Barabara Ya 11
Graham Poll Ayakubali Mabao Ya Arsenal