Kocha mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans, Hans Van der Pluijm amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa lazima APR ya Rwanda ifungashiwe virago katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, lakini watakaokuja mbele yao nao lazima wakalishwe.

Pluijm anasema Al-Ahly ni klabu yenye kikosi cha kawaida na wala haamini kama kina ukali kama kinavyozungumzwa katika kila kona ya barani Afrika.

Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, ameonyesha kushangazwa na hatua ya mashabiki wengi wa soka nchini, kuizungumzia sana Al-Ahly na kuwaacha Clube Recreativo Desportivo do Libolo ambao pia wana nafasi ya kukutana na young Africans kwenye hatua inayofuata.

Young Africans itarudiana na APR mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, nayari inaaminiwa itakuwa kazi nyepesi kwa wawakilishi hao wa Tanzania kutokana na ushindi wa mabao mawili kwa moja waliouvuna jijini Kigali mwishoni mwa juma lililopita.

Young Africans, pia itakuwa na faida ya kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, ambapo kutakua na sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki ambao wanatarajiwa kufuruka uwanjani siku hiyo.

Mabingwa hao wa Tanzania bara endapo watavuka hatua hiyo, watakutana na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri au Clube Recreativo Desportivo do Libolo ya Angola, timu hizo zilitoka suluhu 0-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Angola, mwishoni mwa juma lililopita.

Young Africans, inawafahamu vizuri Al-Ahly na iliwakosa kosa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 2013, kama si Said Bahanuzi kukosa penati.

Balozi Mwapachu: Nililewa Mahaba ya Lowassa na ahadi yake kwangu, nilikosea
Emmanuel Petit: Arsene Wenger Anapaswa Kuondoka