Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amesaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomfanya kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye makazi yake jijini London mpaka ifikapo mwaka 2023.

Tangu ajiunge na Tottenham mwaka 2014 kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 ameiwezesha klabu hiyo kumaliza msimu ikiwa katika nafasi nne za juu katika msimu mitatu mfurulizo.

Tottenham wanapanga kuanza kuujenga upya uwanja wao wa White Hart Lane baada ya msimu uliopita kuutumia uwanja wa Wembley kama uwanja wao wa nyumbani.

Baada ya kusaini mkataba mpya utakaomfanya kuweka mfukoni kiasi cha paundi milioni 8.5 kila mwaka Pochettino tayari ameonyesha nia ya kutaka kuimarisha kikosi chake akiwa nataka kuwasaini mshambulajia wa Manchester United mfaransa Anthony Martial, beki wa Ajax mholanzi Matthijs de Ligt, winga wa Fuljham Ryan Sessegnon na winga wa Cyrstla Palace Wilfried Zaha.

 

Babu Tale arudi uraiani
Serikali kushusha faini za bodaboda julai