Kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba huenda akaanzia Benchi wakati Manchester United itakapovaana na Tottenham Hotspur ugenini leo usiku, kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England (PL).

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema hana papara ya kutaka kulazimisha kumuanzisha Pogba ambaye ndio ameanza kuwa fiti, baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majera ya goti.

Badala yake meneja huyo kutoka Norway amepanga  kuwaanzisha viungo, Bruno Fernandes, Fred, Scot McTominay na Nemanja Matic.

Inatajwa kuwa Solskjaer ameamua hivyo ili kumpa muda zaidi Pobga kujiweka sawa,  ili amtumie sambamba na kiungo Bruno Fernandez ambaye amegeuka kipenzi cha mashabiki wa Manchester United.

Wakati Pogba akitarajiwa kuanzia benchi, upande wa pili wao wataendelea kumkosa kiungo wao Delle Alli ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kwa kitendo cha utovu wa nidhamu alichokionyesha miezi mitatu iliyopita.

Chama cha Soka England (FA) kilimfungia Alli kwa kosa la kumkejeli raia mmoja wa Asia juu ya masuala ya Virusi vya Corona.

Kocha wa Tottenham, Jose Mourinho alisema kuwa kiungo huyo ameonewa: “Sidhani kama anastahili adhabu ya kufungiwa mechi moja.
Sio vyema kumuadhibu mtoto ambaye ameshakiri kosa. Huwa sipendi hii migongano,” alisema Mourinho.

Timu hizo zinakutana leo wakati Spurs wakiwa nafasi ya nane na pointi zao 41 wakati United wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 45.

Jaji mkuu achambua uhuru wa Mahakama
TAKUKURU yamnasa Salum Mkemi