Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ameeleza mkakati wake mkuu ndani ya chama hicho ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe.

Akizungumza jana katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho zilizoko mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Polepole alimshukuru Katibu wa Itikadi na Uenezi aliyemaliza muda wake, Nape Nnauye na kutangaza mkakati wake kuwa ni kuhakikisha chama hicho kinajikita katika kuwatetea wanyonge.

“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.

Alisema kuwa atajikita katika mkakati huo kwani ndio msingi hasa wa kuwanzishwa kwa chama hicho ambao hatauacha.

Aidha, Polepole alisema ingawa kazi yake ni kuratibu Itikadi na Uenezi, atajikita zaidi katika itikadi kwani ndiyo inayokibeba chama.

Katika hatua nyingine, Mwanasiasa huyo aliyejipatia umaarufu nchini wakati wa uanzishwaji wa mchakato wa kupata katiba mpya akiwa mmoja kati ya Wajumbe wa Tume ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Jaji (mstaafu) Joseph Warioba, alisema kuwa Nape alifanya kazi nzuri katika kipindi chake na kwamba ataendelea kumuomba ushauri.

Afande Sele aanika sababu za kuitosa ACT Wazalendo
Marekani yathibitisha Putin alisaidia kumpa ushindi Trump kupitia udukuzi