Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amekanusha taarifa za chama hicho kumpa barua ya onyo Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Polepole amesema mbunge huyo wa CCM hajapewa barua ya onyo, na kwamba chama hicho kina taratibu zake.

“Chama chetu kina utaratibu wa vikao, sio kutoa barua tu,”

Zimekuwa zikisambaa taarifa za Nape kupewa barua hiyo mitandaoni huku mwenyewe akikanusha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Moja ya sababu za kusambaa taarifa hizo ambazo zimekanushwa ni baada ya kuhusishwa na msimamo wake katika suala la Korosho lililoibuka katika Bunge la Bajeti.

Hivi karibuni katika mkutano huo wa Bunge, Nape na wabunge wenzake kutoka mikoa ya Kusini walipinga uamuzi wa Serikali wa kubadilisha Sheria ya Korosho, ikiwa ni pamoja na fedha za ushuru wa korosho kwenda katika mfuko mkuu wa hazina.

Muna amtaja baba halali wa mtoto wake Partick, 'Shetani alinipitia'
Simba yamleta kocha mpya kimyakimya

Comments

comments