Leo April 22, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amewataka baadhi ya watu wanamtuhumu Rais wakidai amelisababishia Taifa hasara kuacha mara moja kwani hawana uthibitisho wa kauli hiyo.

Polepole amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameandika;

“Ukimtuhumu Rais amelisababishia hasara Taifa ukaombwa uthibitishe utaweza au utasema yalikuwa tu majadiliano ya twita baada ya chakula cha mchana?”

“Huko barabarani defamation ni kosa kubwa, lakini mbona mnataka viongozi wetu wadhalilishwe kisha tukae kimya, kaanze kumtukana babako” -Polepole.

Defamation ni neno na kosa kisheria likimaanisha sentensi au tuhuma za uongo ambazo mtu husema au huandika juu ya mtu mwingine.

 

Abdu Kiba afuata nyendo za kaka yake
Picha: Mwili wa Masogange ukitolewa Muhimbili na kupelekwa Leaders kwa kuagwa

Comments

comments