Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa kitendo cha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad kuliita Bunge ni dhaifu ni kukikosea heshima chombo hicho kilichopewa mamlaka kamili.

Ameyasema hayo zikiwa zimesalia siku chache kufika Januari 21 ambayo Mkaguzi huyo ametakiwa na Spika wa Bunge kwenda kuhojiwa na Kamati ya Maadili.

Aidha, amesema kuwa watu wanapaswa kusoma Katiba ili kujua hata tabia mbaya inaweza kumuondoa mtu katika nafasi yake bila kujali cheo alicho nacho.

“Mimi nataka watu wasome tu Katiba, tabia mbaya inaweza kufanya Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali anaweza kuondolewa kwenye nafasi yake. Sijasema ana tabia mbaya hapana! Nimesema kwamba tuheshimu Katiba. na tusipuuza mambo, na tusizushe mambo ambayo hayapo. Si kitu kizuri,”amesema Polepole.

Hata hivyo, Polepole ameongeza kuwa yeye amekuwa shuhuda wa vitu vya serikali vikifanyiwa kazi bungeni, na pia kutokana na kazi zao wanapaswa kukumbushwa, kutiwa moyo na si kuwasema kuwa ni dhaifu.

Video: Matefu amshauri CAG kuitikia wito wa Spika wa Bunge
Aweso azindua mradi wa maji mkoani Kagera

Comments

comments