Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesemshukia waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa alishindwa kumshawishi Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete kuhusu sakata la Nguza Viking (Babu Seya) na wanaye.

Polepole amesema kuwa kwakuwa Lowassa alikuwa Waziri Mkuu, alikuwa na nafasi ya kumshawishi Dkt. Kikwete kuisamehe familia ya mwanamuziki huyo kama aliona inafaa kufanya hivyo lakini alishindwa kutumia nafasi yake kufanya hivyo.

Aidha, alimtaka kuachana na madai ya kuwa ndiye aliyeahidi kuwatoa wanamuziki hao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Kashindwa kuzuia Babu Seya asifungwe, kashindwa mwaka wa kwanza kumshawishi Rais wake amsamehe Babu Seya, ameshindwa kufanya hivyo kwa miaka mingi iliyopita,” alisema.

“Magufuli hakuwa kwenye nafasi ya uamuzi kipindi hicho alikuwa Waziri wa kawaida kabisa baada ya tafakuri ya kina ya miaka miwili akaona katika watu ambao wamejirudi huyu anastahili msamaha, huyo mzee anaibuka oohh nilifanya mimi, huyu mzee aache hizi tabia za kinafiki, kizandiki kwani Watanzania wanataka upinzani unaojenga hoja,” aliongeza.

Rais John Magufuli alitangaza wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania Bara kuwasamehe Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, ikiwa ni miongoni mwa wafungwa aliowasamehe waliokuwa wakitumikia vifungo vya maisha na adhabu ya kunyongwa.

Babu wa Loliondo adai ameoteshwa maelfu watafuata kikombe tena
Amuua mkewe kwa shoka, panga kisa ‘meseji’ ya simu