Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametishia kung’oa kiongozi mkubwa wa Chadema ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

Ameyasema hayo mara baada ya madiwani wawili kuachia ngazi ndani ya Chadema Mjini Iringa, ambapo amesema kuwa hoja za madiwani hao wanakimbia ubabe wa mchungaji Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.

“Nasikia wameambiwa wasimpinge mkubwa wao, nilidhani mkubwa ni wananchi waliowachagua, kumbe ni Mchungaji Msigwa, nitachomoa kiongozi mmoja hapa Dar es salaam,”amenukuliwa Polepole

Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la viongozi wa kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kuhamia chama tawala cha CCM.

 

 

Video: Prof. Beno Ndulu aaga, Kura ya CCM yaipa Ukawa ushindi
Magazeti ya Tanzania leo Januari 4, 2018